Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na wajumbe wa kamati
ya siasa mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha
Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017.
Picha zote Na Mathias Canal
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa akizungumza na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa
Mbeya mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha
Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Katibu wa Chama Cha
Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson Nkambaku mara baada ya kuwasili
kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa
ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017.
Na Mathias Canal, Mbeya
Chama
Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya kimemshukuru na kumpongeza Mhe Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kumteua Mhe
Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo kuhudumu katika nafasi hiyo
katika serikali ya awamu ya tano.
Pongezi
hizo pamoja na shukrani zimetolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi
Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson Nkambaku kwa niaba ya wajumbe wa kamati ya
siasa wakati akitoa taarifa ya chama hicho Ofisini kwake Mara baada ya
Naibu Waziri kuzuru katika Ofisi hizo akiwa ziarani Mkoani Mbeya.
Nkambaku
alisema kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi muhimu kwani Mhe Mwanjelwa
ni mchapakazi na msaada mkubwa kwa chama hicho hivyo uteuzi huo
umeonyesha Imani kwa Chama Cha Mapinduzi na Wananchi wa Mkoa mzima wa
Mbeya.
Aidha
alimsihi Kutenda haki na kufanya kazi kwa bidii huku CCM ikiahidi kutoa
ushirikiano mwema Kwa Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Viti Maalumu
(CCM) Mkoani Mbeya.
Akizungumza
na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake kwenye Ukumbi wa
Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa
aliwasihi makada hao Kutofanya kazi za Chama kwa Mazoea badala yake
kufanya kazi kwa weledi ili kuwasaidia wanachama na wasiokuwa wanachama
wa CCM katika shughuli za maendeleo.
Naibu
Waziri Huyo ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi
Taifa (MNEC) amejivunia malezi bora na muhimu aliyoyapata ndani ya Chama
Cha Mapinduzi huku akiwasihi viongozi kuongeza bidii katika kumsaidia
Rais Magufuli kutimiza ndoto ya Tanzania Mpya kwa manufaa ya watanzania
katika kuwaletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment