Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akizungumza na Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla wakati alipozuru ofisini kwake mara
baada ya kuwasilia mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku, Leo 20
Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-WazoHuru Blog
Picha
ya pamoja Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (katikati)
akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla mara baada ya
mazungumzo wakati alipozuru ofisini kwake akiwa mkoani humo kwa ziara ya
kikazi ya siku mbili, Leo 20 Februari 2018. Wengine pichani ni Mbunge
wa Mbeya Vijijini Oran Njenza CCM (Kulia), Katibu tawala wa Mkoa wa
Mbeya Bi Mariamu Mtunguja (Wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya
Paul Ntinika (Wa kwanza kushoto).
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akisikiliza kwa
makini taafifa kuhusu sekta ya madini kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Mhe Amos Makalla wakati alipozuru ofisini kwake mara baada ya kuwasilia
mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku, Leo 20 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Mbeya
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameanza ziara ya kikazi katika
Mkoa wa Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea kiwanda cha
kutengeneza Samani mbalimbali zinazotokana na Marble, kukagua shughuli
za uchakataji Madini ya malumalu na mradi wa Pandahili (Niobiaum).
Maeneo
mengine atakayotembelea ni pamoja na mgodi wa Sunshine uliopo katika
Wilaya ya Chunya ambapo atazungumza pia na wachimbaji wadogo katika
migodi atakayotembelea.
Mara
baada ya kuwasili katika Mkoa wa Mbeya Mhe Biteko amesifu juhudi za
Mkuu wa Mkoa huo Mhe Amos Makalla kwa uthubutu mkubwa katika utendaji
ikiwa ni pamoja na usimamizi madhubuti katika sekta ya Madini.
Pamoja
na pongezi hizo Mhe Biteko amemsihi Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya kuongeza
juhudi zaidi ili kutimiza ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuwatumikia watanzania na
kupelekea kunufaika na rasilimali zao ikiwemo sekta ya Madini.
Alisema
kuwa Sekta ya Madini bado ni muhimu hivyo inahitaji kulelewa ili ikuwe
na hatimaye kuongeza ufanisi katika uchangiaji wa pato la Taifa
Alisema
kila kiongozi ana wajibu mkubwa kuwa mbunifu katika uwajibikaji wake
huku akiongeza kuwa Jukumu la msingi la kiongozi ni pamoja na kutafsiri
ndoto za Rais Magufuli ili kuwafanya wananchi kunufaika na uongozi bora
na utendaji wa serikali ya awamu ya tano.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makala amesisitiza
kuendeleza ushirikiano madhubuti na Wizara ya Madini ili wananchi Mkoani
humo wanufaike na matunda ya kukichagua Chama Cha Mapinduzi kuongoza
dola.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment