Nyumba moja iliyopo eneo la Sae Mbeya imenusurika kuungua kwa moto mchana huu, huku majirani wakidai chanzo chake kimesababishwa na hitirafu ya umeme.
Majirani waliokuwepo katika tukio hilo walidai kuwa waiona moshi ukifuka katika bati na ndipo walipo sogelea nyumbani hapo na kukuta tayari baadhi ya vitu yakiwemo masofa, Tv, Radio na vyenginevyo vimeanza kuwaka moto na juhudi za kuokoa zikaanza.
Mpaka tunaondoka eneo la tukio tayari wasamalia wema walikuwa wamesha uzima moto.
Baadhi ya vitu vilivyopona baada ya moto huo kuzimwa
Moja ya Sofa likiwa limeungua kutokana na moto huo
Radio, Tv, Kabati pamoja na vitu mbalimbali vikiwa vimeungua
Hii ni sehemu ya nyumba iliyotaka kuwaka moto
Picha na Blogs za Mikoa






No comments:
Post a Comment