Social Icons

Featured Posts

Monday, February 26, 2018

JUST IN: MBUNGE WA MBEYA JOSEPH MBILINYI 'SUGU' KAHUKUMIWA MIEZI MITANO JELA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imewatia hatiani mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga na kuwahukumu kifungo cha miezi mitano jela.

Hukumu hiyo imetolewa leo Februari 26,2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Michael Mteite.

Sugu na Masonga wamehukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Kwa Hisani ya Kijukuu cha Bibi K

Friday, February 23, 2018

MHE BITEKO AWATAKA WAMILIKI WA LESENI KUIGA MFANO WA KIWANDA CHA KUKATA NA KUSUGUA MAWE CHA MARMO KATIKA UONGEZAJI THAMANI YA MADININaibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua  mawe yaliyo katwa, Kusagwa na kuongezewa thamani katika kiwanda cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal, Wazo Huru Blog
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko  akiwasili katika kiwanda kinachoshughulika na kukata, Kusaga na kuuza mawe cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Ndg Salim Jesa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Marmo E. Granite Mines (T) Ltd kuhusu usafirishaji wa mawe baada ya kuyaongezea thamani wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua  utendaji kazi wa kiwanda cha kukata, Kusaga na kuuza mawe cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.

Na Mathias Canal, Mbeya

Wamiliki wa leseni za madini ya dhababu, vito na mengineyo kote nchini wametakiwa kuiga mfano wa Ndg Salim Jesa mmiliki wakiwanda cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd kinachojishughulisha na kukata, Kusaga na kuuza mawe kwa kufanya mchakato mzima mpaka bidhaa kukamilika hapa hapa nchini.

Kauli hiyo kwa wamiliki wa leseni za madini nchini imetolewa leo 20 Februari 2018 na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya.

Alisema kuwa kiu ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ni kuona rasilimali za nchi zinaongezwa thamani zikiwa ndani ya nchi jambo ambalo linaakisi umakini wa utendaji na ulipaji kodi ya serikali pasina kukwepa ama kutorosha rasilimali madini yakiwa ghafi.

Aliseama kuwa faida ya kuongeza thamani ya madini nchini ndio muarobaini wa sekta ya madini kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la Taifa hatimaye kufikia asilimia 10% kama ulivyo mpango wa wizara kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la Taifa.

“Nchi nyingi ambazo zimejua siri hii kwa kiasi kikubwa zimefanikiwa lakini sisi Tanzania tulichelewa sana, na kama tungeendelea kuchelewa ingefika kipindi ambacho madini yasingekuwepo kamwe na kama Taifa tungeambulia mashimo makubwa na kusalia katika wimbi la umasikini” Alisema Mhe Biteko

Aidha, amemuhikishia mmiliki wa kiwanda hicho kuwa serikali itazungumza na taasisi zinazofanya kazi za ujenzi nchini kuunga mkono juhudi za umahiri wa kiwanda hicho kwa kununua bidhaa zinazozalishwa hususani wakati huu ambao serikali inaendelea na mchakato wake wa kuhamia Mjini Dodoma.

Sambamba na hayo pia uongozi wa kiwanda hicho umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweka sera nzuri hususani kwa wawekezaji wa ndani katika sekta ya madini na juhudi zake za kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na serikali kwa ujumla wake.

Kampuni ya Marmo E. Granite Mines (T) Ltd iliyopo mkoani Mbeya ilianzishwa mradi wa kukata, kusaga na kuuza mawe Januari 2004 baada ya kukidhi masharti ya usajili wa makampuni.

Tuesday, February 20, 2018

MHE BITEKO AANZA ZIARA MKOANI MBEYA AMPA HEKO RC MAKALLA USIMAMIZI WA SEKTA YA MADINI


Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla wakati alipozuru ofisini kwake mara baada ya kuwasilia mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku, Leo 20 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-WazoHuru Blog
Picha ya pamoja Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (katikati) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla  mara baada ya mazungumzo wakati alipozuru ofisini kwake akiwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, Leo 20 Februari 2018. Wengine pichani ni Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njenza CCM (Kulia), Katibu tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi Mariamu Mtunguja (Wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika (Wa kwanza kushoto).

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akisikiliza kwa makini taafifa kuhusu sekta ya madini kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla wakati alipozuru ofisini kwake mara baada ya kuwasilia mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku, Leo 20 Februari 2018.

Na Mathias Canal, Mbeya

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea kiwanda cha kutengeneza Samani mbalimbali zinazotokana na Marble, kukagua shughuli za uchakataji Madini ya malumalu na mradi wa Pandahili (Niobiaum).

Maeneo mengine atakayotembelea ni pamoja na mgodi wa Sunshine uliopo katika Wilaya ya Chunya ambapo atazungumza pia na wachimbaji wadogo katika migodi atakayotembelea.

Mara baada ya kuwasili katika Mkoa wa Mbeya Mhe Biteko amesifu juhudi za Mkuu wa Mkoa huo Mhe Amos Makalla kwa uthubutu mkubwa katika utendaji ikiwa ni pamoja na usimamizi madhubuti katika sekta ya Madini.

Pamoja na pongezi hizo Mhe Biteko amemsihi Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya kuongeza juhudi zaidi ili kutimiza ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuwatumikia watanzania na kupelekea kunufaika na rasilimali zao ikiwemo sekta ya Madini.

Alisema kuwa Sekta ya Madini bado ni muhimu hivyo inahitaji kulelewa ili ikuwe na hatimaye kuongeza ufanisi katika uchangiaji wa pato la Taifa 

Alisema kila kiongozi ana wajibu mkubwa kuwa mbunifu katika uwajibikaji wake huku akiongeza kuwa Jukumu la msingi la kiongozi ni pamoja na kutafsiri ndoto za Rais Magufuli ili kuwafanya wananchi kunufaika na uongozi bora na utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makala amesisitiza kuendeleza ushirikiano madhubuti na Wizara ya Madini ili wananchi Mkoani humo wanufaike na matunda ya kukichagua Chama Cha Mapinduzi kuongoza dola.

MWISHO.

Friday, February 16, 2018

SERIKALI KULIPA FIDIA WANANCHI UJENZI WA BANDARI ZA ZIWA NYASA


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akiteremka kwenye boti katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya
Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri Sese (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) wakati wa ziara yake kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Deo Ngalawa na wa kwanza kushoto ni Katibu wa Mhe. Nditiye Mhandisi Hamza Faiswary.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyeketi) akisimikwa kuwa Chifu wa kitongoji cha Ihiiga kilichopo kwenye kijiji cha Nkwimbili, kata ya Lupingu, Wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe ikiwa ishara ya pongezi kwa kiongozi wa kitaifa kufika hapo tangu mwaka 1979 katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya. Wa kwanza kushoto ni mzee Thadei Otmari Ngalawa na aliyevaa miwani ni Diwani wa Kata ya Lupingu Mhe. Skanda Mwinuka.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nsele kilichopo kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoani Njombe katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa Mzee Kolimba akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda wilaya ya Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya

………………….

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga shilingi milioni 358 kwa ajili ya kulipa fidia nyumba na ardhi za wananchi waishio mwambao wa Ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari za Ziwa hilo

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake aliyoifanya ya kukagua bandari za Ziwa Nyasa kuanzia bandari ya Manda iliyopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe hadi bandari ya Itungi iliyopo wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.

Katik ziara hiyo, Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri Msese amesema kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania imetenga fedha hizo kwa ajili ya kulipa fidia wananchi wa maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa waliojitolea maeneo yao ili kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari zilizopo ndani ya Ziwa Nyasa kuanzia bandari ya Lipingu iliyopo Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe hadi bandari ya Matema iiyopo wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Naye Mkuu wa Wilaya wa Ludewa Bwana Andrea Tsere amemueleza Mhandisi Nditiye kuwa tayari wamekamilisha kazi ya kuhakiki malipo ya fidia za wananchi waliotoa ardhi zao eneo la Manda na Lupingu. “Wanachi wa eneo la Manda watalipwa shilingi milioni 192 ambapo wametoa eneo la ukubwa wa hekari 24 na wa Lupingu wametoa eneo ukubwa wa hekari 10.6 na watafidiwa shilingi milioni 166, amesema Tsere”.

Bwana Msese amesema kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania inakamilisha ujenzi wa meli ya mizigo na abiria na itaanza kazi ya kusafirisha abiria na mizigo ndani bandari za Ziwa Nyasa mwezi Agosti mwaka huu ambapo meli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria mia mbili na mizigo tani mia mbili kwenye jumla ya bandari kumi na tano zilizopo ndani ya mwambao wa ziwa Nyasa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Deo Ngalawa amemshukuru Mhe. Mhandisi Nditiye kwa niaba ya wananchi wake kwa kufika kwenye makazi ya wananchi hao waishio kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa na kukagua mahitaji ya usafiri wa majini wa abiria na mizigo wa Ziwa hilo ambapo Serikali tayari imetenga fedha kulipa fidia wananchi waliotoa maeneo yao kupisha ujenzi na upanuzi wa bandari za Ziwa hilo.

Ujenzi wa bandari hizo na utoaji wa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo ni ukamilishaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa wananchi waishio kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa ambao wanategema Ziwa hio kwa kiasi kikubwa kwa shughuli za kiuchumi, biashara na kijamii ambazo zitachangia ukuaji wa uchumi wa wananchi hao na taifa kwa ujumla.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano

Friday, January 26, 2018

Hakimu agoma kujitoa, mawakili wajitoa kesi ya Sugu


Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite amekataa kujitoa kusikiliza kesi inayomkabili mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na mwenzake.
Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli wanayodaiwa kuitoa Desemba 30,2017.
Awali, leo Alhamisi Januari 25,2018 Sugu na Masonga waliwasilisha ombi mahakamani wakimkataa hakimu huyo wakitaka ajitoe kusikiliza kesi kwa maelezo kuwa hawana imani naye.
Hakimu Mteite amesema sababu zilizotolewa na akina Sugu hazipo kisheria na hazimfanyi kujitoa.
Baada ya hakimu kukataa kujitoa, mawakili Boniface Mwabukusi, Hekima Mwasipu na Sabina Yongo wanaowawakilisha washtakiwa walitangaza kujitoa katika shauri hilo.
Sugu na Masonga wameiomba Mahakama kuwapatia wiki mbili za kutafuta mawakili wengine.
Hakimu Mteite ameahirisha kesi hadi Februari 2,2018 na ameamuru washtakiwa kurejeshwa rumande.

Chanzo: Mwananchi