Mtaalamu wa Sosholojia Bi. Vaileth Kimaro akizungumza na vikundi vya wanawake wakati wa kujibu maswali na kupokea maoni kuhusu athari na faida za mradi wa jotoardhi wa Ngozi kwa jamii na mazingira.
Mhandisi
Leonard Masanja (aliyesimama kushoto) akijibu hoja za wananchi wa Kata ya Ndanto
wakati wa mjadala wa athari na faida za mradi wa jotoardhi wa Ngozi kwa jamii
na mazingira, aliyeshika kipaza sauti ni Afisa Maendelea ya Jamii wa Wilaya ya
Rungwe Bi. Rachel Mbelwa
Na Johary Kachwamba -TGDC
Wananchi wa Wilaya za Rungwe na
Mbeya Vijijini pamoja na wadau wengine wa mradi wa jotoardhi wa Ngozi wametoa maoni mbalimbali ikiwa ni
pamoja na kuuliza maswali ya msingi kabla ya zoezi la uchorongaji visima vya
uchunguzi na baadae uvunaji mvuke wa kuzalisha umeme utakaotokana na nishati ya
jotoardhi.
Wananchi walipata fursa ya kutoa
maoni yao kati ya tarehe 6 hadi 11 Machi, 2017, wakati timu ya wataalamu wa
Mazingira na Jamii kutoka Kampuni ya kuendeleza Jotoardhi Tanzania (TGDC) na
TANESCO walipotembelea eneo la mradi, ikiwa ni matakwa ya kisheria ya kushirikisha
wadau na jamii itakayopitiwa na mradi husika, wakati wa kufanya tathmini ya
athari za mradi katika mazingira na jamii.
Maoni yao ilikuwa ni pamoja na kuiomba
Serikali kusimamia taratibu za ajira wakati wa zoezi la uchorongaji visima vya
jotoardhi, akizungumza Ndugu Yohana Julius wa Kata ya Swaya Vijijini alisema “wanaomba
ajira zisizohitaji ujuzi wapatiwe wakazi wa eneo la mradi ili wanufaike moja
kwa moja kwa kujiongezea kipato”
Bibi Mary Gwamaka alisema “wanaomba
mradi huu usiwaache nyuma wakina mama, kwani wanao uwezo wa kufanya kazi
mbalimbali, hivyo wanaomba wasibaguliwe”
Akijibu moja ya maswali ya wananchi,
Mhandisi wa Mazingira kutoka TANESCO Bw. Fikirini Mtandika alisema sheria na
taratibu zote za mazingira zitazingatiwa wakati wote wa utekelezaji wa mradi
chini ya usimamizi wa Baraza la Udhibiti na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira.
“TGDC inaandaa mikakati mbalimbali
ya kupunguza na kuziondoa kabisa baadhi ya athari za mradi huu katika mazingira
yetu” aliongezea Mhandisi Mtandika.
Wananchi wa maeneo yote yanayozunguka
mradi wa jotoardhi wa Ngozi wameridhia hatua ya uchorongaji visima vya
uchunguzi na baadae uzalishaji umeme na wako tayari kutoa ushirikiano. Kata zinazopitiwa
na mradi huu ni Ijombe, Swaya-Mbeya vijijini, Swaya Rungwe na Ndanto.
No comments:
Post a Comment