Mashamba ya mpunga ya Mbarali Highland Estates, Kapunga Rice Project, Kapunga Small
Holders farm, pamoja na skimu za umwagiliaji za Mwanavala (Nguvukazi
farm), Mwashikamile pamoja na Sikimu ya
Mwendamtitu zilizoko Mbarali mkoa wa
Mbeya yametozwa faini ya jumla ya kiasi
cha shilingi 120,290,000/= baada ya
kukiuka sheria mbalimbali za Mazingira zilizo chini ya Baraza la Usimamizi wa
Mazingira (NEMC).
Faini hiyo inayotakiwa kulipwa ndani ya siku kumi na nne
kuanzia tarehe 27 aprili 2017, imetozwa
na Kikosi Kazi cha Kitaifa cha kuokoa
Ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu kilichoko Mkoani Mbeya kupitia kwa Mwananasheria wa
NEMC- Vicent Haule , baada ya kugundua
makosa mbalimbali ya uvunjifu wa sheria za mazingira na umwagiliaji katika
Mashamba hayo wakati wa ziara ya kutembelea mashamba ya Mpunga na skimu tofauti
za umwagiliaji wilayani humo.
Akiongea na Waandishi
wa Habari Mwenyekiti wa Kikosi kazi hiko cha Kitaifa Bwana Richard Muyungi, alisema kwamba kutokana
na makosa mbalimbali yaliyokutwa katika
masahamba hayo ikiwemo kutokuwa na vyeti vya ukaguzi wa Mazingira, kukiuka
taratibu za umwagiliaji kwa kutoa na
kutumia maji bila ruhusa, kuweka
mifereji mikubwa ya kumwagilia mashambani pasipo kufuata sheria na
kanuni zinazotakiwa, kutorekebisha miundombinu ya Umwagiliaji kwa mifereji ya
kutolea maji. Mashamaba hayo yanapigwa faini kama ifuatavyo Mbarali Estates
33,000,000, Kapunga Rice Project 33,100,000/=, Kapunga Small Holders
3,000,000/=, Madibila farm Project 33,000,000. Pamoja na mashamba hayo pia zipo
skimu za Umwagiliaji zilizotozwa faini ikiwepo Skimu ya Mwendamtitu 7,995,000, Mwanavala (Nguvukazi)
7,995,000/=, Mwashikamile 2,200,000/=.
Aidha aliongeza pia mashamba ya Mwashikamile,
Mwanavala(nguvu kazi) na Kapunga Small Holders, wanatakiwa kulipa faini lakini pia baada ya kuvuna wanatakiwa kuacha mara moja kulima tena
katika mashamba hayo mpaka pale watapofuata taratibu za kupata vibali vya maji
na cheti cha ukaguzi wa mazingira kutoka NEMC na Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji
."Kutoza faini hizi siyo kukomoa Mashamba haya ila ni kuhakikisha kuwa
Wamiliki wa mashamaba makubwa ya umawagiliaji wote Nchini wanafuata taratibu
na Sheria za kimazingira katika
kuendesha mashamba haya" alisema Muyungi
Kikosi kazi hiko kiko MKoani Mbeya kwa kukagua na kutembelea
sehemu mbalimbali za mashamba , skimu za
umwagiliaji na pia kusikiliza maoni ya Wananchi jinsi ikiwa ni harakati za
kurudisha ikolojia ya mto Ruaha.
No comments:
Post a Comment