Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene
LICHA ya sekta ya madini kutajwa kuwa kinara katika uchangiaji wa
Pato la Taifa, serikali imesema sekta ya kilimo inapaswa kushika namba
moja kutokana na kuhusisha watu wengi kwenye uzalishaji wake.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene (pichani) alipokuwa
akitoa hotuba ya kufunga maonesho ya sherehe za Wakulima (Nanenane)
kwenye Uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya kwa niaba ya Makamu wa
Rais, Samia Suluhu.
Simbachawene alisema kilimo ni namba moja katika uchangiaji wa Pato
la Taifa kutokana na kuhusisha watu wengi na kutoa ajira ya moja kwa
moja kuanzia ngazi ya uzalishaji, uongezaji wa thamani na wakati wa
kuuza bidhaa zake.
Alisema pia sekta ya kilimo ndiyo msingi na shabaha ya serikali
katika kuepukana na njaa kwani kupitia sekta ya kilimo inayohusisha
idara ya mifugo, uvuvi, nyuki, misitu na kilimo, kunafanya kuondokana na
umasikini ili kufikia uchumi wa viwanda. Aliongeza kuwa mwaka huu kuna
ziada ya chakula kwa asilimia 20 huku mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
ikiwa ndiyo kinara kwa uzalishaji kutokana na fursa ya hali ya hewa
nzuri wanayoipata, nguvu kazi.
CHANZO HABARI LEO
No comments:
Post a Comment