Moto huo ukiendelea kuteketeza bidhaa mbalimbali zilizomo sokoni humo.
Moto huo ukiendelea kuteketeza bidhaa mbalimbali zilizoachwa sokoni hapo, huku Kikosi cha Zima Moto kikiendelea kupambana nao.
Moto huo ukiendelea kuteketeza bidhaa mbalimbali zilizoachwa sokoni hapo
Taarifa
zilizotufikia hivi punde kutoka kwa Ripota wetu jijini Mbeya,zinaeleza
kuwa Soko la Sido lililopo mkabala na maeneo ya Mwanjelwa linateketea
kwa moto hivi sasa,Taarifa zinaeleza kuwa chanzo cha moto huo bado
hakijajulikana mpaka sasa.
Kwa
mujibu wa Ripota wetu aliyepo eneo la tukio, moto huo ulianza kuwaka
mnamo majira ya saa tatu usiku na kusababisha tafrani kubwa kwa watu
waliokuwepo maeneo hayo, ambao nao walionesha juhudi zao za kushriki
kuuzima, kwa bahati nzuri kikosi cha zima moto kikawasili na kupambana
na moto huo uliokuwa ukiwaka kwa kasi kubwa.
Katika
kuongeza nguvu za usalama eneo hilo, kikosi kutoka Jeshi la Polisi la
mjini Mbeya liliwasili katika eneo hilo katika kuhakikisha ulinzi na
usalama wa mali za watu unaimarika .
TAARIFA ZAIDI TUTAWALETEA



No comments:
Post a Comment