Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka nchini Malawi wakiwa
wanapumzika baada ya kupanda Mlima Rungwe mpaka kituo cha kwanza cha mapumziko, lengo
la ziara hiyo ikiwa ni kujifunza jinsi Wakala wa Huduma Misitu Tanzania (TFS) wanavyofanya suala la
uhifadhi kwa kuwashirikisha wananchikatika kuzilinda hifadhi hizo.
Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka nchini Malawi wakiwa
wanapanda Mlima Rungwe ambapo waliweza kupanda mlima huo mpaka kituo cha kwanza cha
mapumziko
Wabunge wa Kamati ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka nchini Malawi wamefanya ziara ya mafunzo kwenye Msitu wa asili wa Hifadhi wa Mlima Rungwe mkoani Mbeya na kujionea jinsi wananchi wanavyoshirikishwa katika uhifadhi wa pamoja.
Akizungumza Mwenyekiti wa kamati hiyo, Welani Chilenga amesema lengo la ziara hiyo ni kutaka kujifunza
jinsi Wakala wa Huduma Misitu Tanzania (TFS) wanavyofanya uhifadhi kwa kuwashirikisha wananchi katika
kuzilinda hifadhi zao.
Amesema nchini Malawi wao wamekuwa wakitumia mitutu katika kulinda Misitu jambo ambalo halijawawezesha
kufanikiwa katika uhifadhi hivyo sehemu kubwa ya miti yao imekatwa.
Chilenga amesema wamejionea vyanzo vya maji ambapo mlima huwa ni chanzo cha mito 21 na wameiomba TFS
kuendelea na juhudi za uhifadhi kwani nao wamekuwa wakifaidika na Mlima huo kama chanzo chao cha maji
kupitia ziwa Nyasa
Katika hatu nyingine, Wabunge wa Kamati hiyo walifanikiwa kupanda mlima huo mpaka kituo cha kwanza cha
mapumziko.
Awali, Mhifadhi Mkuu wa Mlima Rungwe, Innocent Lupembe amewataka watanzania kutembelea hifadhi hiyo ili
waweze vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi hiyo wakiwemo ndege na wanyama wa aina mbali
mbali.
Aidha, Aliwataka watafiti wa ndani na nje ya nchi wafanye tafiti katika hifadhi hiyo kwa kuwa ina amali ambayo
haipatikani mahali popote pale duniani nisipokwa katika Mlima huo.


No comments:
Post a Comment