Na
Bashir Yakub.
1.UKOROFI WA
WASIMAMIZI WA MIRATHI.
Baadhi ya
wasimamizi wa mirathi
ni wakorofi. Baada
ya kuteuliwa kwa
jukumu hilo hawapendi
kugawa mali ili kila
mtu achukue chake. Inapaswa kufahamika
kuwa mali si
za msimamizi wa
mirathi . Mali ni
za warithi halali
isipokuwa msimamizi ni
kiongozi tu. Kwa
maana hii anawajibika
kusikiliza warithi wanasema
nini ili mradi
kile wanachosema kisipingane na sheria.
Wakati mwingine warithi
wanataka wagawiwe mali
zao ili kila
mtu endelee na
maisha yake lakini msimamizi
hataki tena bila
sababu za msingi. Hili
linakuwa si sawa
isipokuwa kama kuna sababu
za msingi za kufanya
hivyo.
Sababu zaweza kuwa labda
anayetaka kugawiwa mali ni mtoto
mdogo asiyeweza kumiliki mali kwa wakati huo, ni
mtu asiye na akili
timamu kwa muda huo,
kuna shauri mahakamani kuhusu hiyo
mirathi linaendelea, mali hazijakusanywa zote, kuna
ugomvi kwa warithi
kuhusu mali ambao
utaathiri mgao nk.
2. WAJIBU MKUU WA
MSIMAMIZI WA MIRATHI.
Kifungu cha
108(1) cha Sheria
ya Usimamizi na
Uendeshaji wa Mirathi,
Sura ya 352 kinaeleza wajibu
wa jumla wa msimamia
mirathi. Kifungu kinasema kuwa
kazi kubwa ya
msimamizi wa mirathi
ni kukusanya, mali na
madeni ya marehemu,kutunza mali
hizo, kusimamia gharama za
mazishi na msiba, na
kugawa mali kwa wanaostahili. Na kazi
hii yote ifanyike kwa
uadilifu mkubwa.
Kwahiyo kumbe moja
ya kazi ya lazima
na ya kisheria ya
msimamizi wa mirathi ni
kugawa mali kwa warithi.
Huu ni wajibu
ambao msimamizi anawajibika
kuutekeleza. Na atagawa kwa
mujibu wa wosia
au sheria husika kama hakuna
wosia. Hagawi anavyotaka yeye. Nani
apate nini halipo
katika hiari yake.
KUSOMA ZAIDI
sheriayakub.blogspot.com
No comments:
Post a Comment