Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati
wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya
Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu
kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017. Picha zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati
wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya
Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu
kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati
wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya
Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu
kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
Baadhi
ya wakazi wa Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya wakimsikilkiza Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akitoa maelekezo ya
serikali kuhusu zao la Pareo akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mhe Oran Njeza akizungumza katika mkutano
huo kufikisha kilio cha wananchi mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe
Mary Mwanjelwwa kuhusu zao la Pareto na matatizo la wafanyabiashara
kujaza Lumbesa kwenye uuzaji wa mazao mbalimbali likiwemo zao la viazi
wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijijini Jojo Kata ya Santilya,
Jana Novemba 29, 2017.
Baadhi
ya wakazi wa Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya wakimsikilkiza Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akitoa maelekezo ya
serikali kuhusu zao la Pareo akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
Na Mathias Canal, Mbeya
Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Jana Novemba 29, 2017
amemuagiza Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kumsimamisha
kazi Afisa Kilimo Wilaya ya Mbeya anayesimamia zao la Pareto Ndg
Emmanuel Halinga ili kupisha uchunguzi.
Mhe
Naibu Waziri ametoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi
Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania mara baada ya Mhe
Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Oran Njeza na Wananchi wote waliokuwepo kwenye
mkutano huo wa hadhara kumrushia shutuma nzito na kumkataa mtaalamu huyo
wa kilimo mbele ya Naibu Waziri.
Alisema
kuwa pamoja na zao hilo la Pareto kuwa la kwanza kwa uzalishaji katika
nchi za Afrika huku likiwa zao la pili kwa uzalishaji Duniani lakini
bado halijamkomboa Mkulima nchini jambo ambalo linaonyesha namna ambavyo
baadhi ya wataalamu Wa Kilimo wameshindwa kutekeleza majukumu yao
ipasavyo.
Alisema
kuwa wataalamu wa kilimo walipaswa kusimamia kwa kiasi kikubwa zao hilo
kwani Pato lake ni wastani wa tani 2000 kwa mwaka sawa na Bilioni 12
mpaka 14 ambapo katika kipindi hili bei ya kuanzia Mkulima analipwa
shilingi 2300 kwa kilo lakini inapanda mpaka shilingi 3300 kulingana na
ubora wa zao hilo ambalo mkulima amelima.
Alisema
kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Wa Jamhuri ya
Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inaamini katika kazi ambazo
matokeo yake yanapaswa kuonekana hivyo Mkulima kushindwa kunufaika na
mazao ya Kilimo ni uzembe wa baadhi ya wataalamu Wa Kilimo
unaosababishwa na kufanya kazi kwa mazoea.
Aidha,
Mhe Mwanjelwa ametoa siku saba kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Pareto
nchini Ndg Lucas Ayo kutoa sababu za kwanini mnunuzi ni mmoja wa zao
hilo jambo ambalo linaonyesha kuwa na harufu ya rushwa au kupelekea
kudumaza solo la zao hilo kwa kuwa na mnunuzi mmoja asiyekuwa na
ushindani.
Ili
kuongeza ufanisi wa zao hilo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa
ameelekeza wakulima Kuanzisha vikundi vya vyama vya ushirika vya msingi
ambavyo vitakuwa na usajili serikalini kwani vitasaidia kuwa na mjadala
wa jinsi ya kuwa na ubora wa zao la pareto jambo litakalopekea kuanzisha
viwanda vidogo ambavyo ni ishara ya kuunga mkono juhudi za Rais
Magufuli kuwa na Tanzania ya Viwanda.
"Mkishaanzisha
tu vikundi vya vyama vya ushirika mtoe taarifa mapema iwezekanavyo na
serikali kupitia mrajisi itatoa Elimu ya ushirika" Alikaririwa Mhe
Mwanjelwa
Ameagiza
zao la Pareto kuwa huru ili mkulima awe huru kuuza kwa mnunuzi
anayemtaka kwani kwa sasa kuna mnunuzi mmoja tu ambaye anajipangia
mwenyewe namna ya kununua zao hilo kwa gharama atakazo pasina kupingwa.
Pia
alielekeza wakulima Kuingia kwenye Kilimo cha mkataba kati yao na Chama
cha msingi (AMCOS) jambo litakalorahisisha kupata mikopo ya Kilimo
kupitia Benki ya Kilimo nchini (TADB).
Kuhusu
Lumbesa, aliwataka wafanyabiashara wa wanaojaza Lumbesa badala ya
kujazwa kilo 100 kwa gunia lakini linajazwa mpaka kilo 120 kuacha haraka
tabia hiyo kwani wanakwenda kinyume na sheria hivyo kwa yeyote
atakayebainika atachukuliwa hatua Kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment