Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wananchi
waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa
Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu
Meya wa Jiji la Mbeya Mhe Fanuel Kyanula ambaye ni Diwani wa Kata ya
Sinde akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara
uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa
katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua hatua
zilizofikiwa katika ujenzi wa Vyumba vya madarasa Shule ya Sekondari
Sinde kabla ya kuzungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018
Baadhi ya wananchi wakimlaki Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa mara baada ya kuwasili
kwa ajili ya Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata
ya Sinde Jana Januari 2, 2018.
Diwani
wa Kata ya Manda Mkoani Mbeya Mhe Newton Mwakijobe akitoa salamu za
wananchi wa Kata yake kwenye mkutano wa wananchi wa kata jirani ya Sinde
kabla ya Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kuzungumza na wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo Jana Januari 2, 2018
Na Mathias Canal, Mbeya
IMEBAINIKA kuwa
tofauti za kiitikadi baina ya madiwani katika Halmashauri nyingi
nchini, zimekuwa ni kikwazo kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo
yenye tija kubwa kwa wananchi.
Tofauti hizo zimekuwa
chanzo kikubwa katika utekelezaji wa miradi inayobuniwa na Halmashauri
husika, au inayoletwa na Serikali Kuu na wafadhili. Mitazamo ya kisiasa,
tofauti ya uwakilishi wa vyama na ubinafsi, ndio sababu kuu.
Katika Halmashauri ya
Jiji la Mbeya inayoongozwa na Meya na Naibu Meya wanaotokana na vyama
vya upinzania hali imekuwa tofauti kwani asilimia kubwa ya madiwani
wanaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli tofauti
kabisa na Halmashauri zingine.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Jana 2 Januari 2018 uliofanyika
katika Mtaa wa Kagwina, Kata ya Sinde Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe
Fanuel Kyanula ambaye ni Diwani wa Kata ya Sinde alisema kuwa utendaji
wa Rais Magufuli ni faida ya watanzania wote hivyo kuna kila sababu ya
wananchi kuunga mkono juhudi za serikali yake.
Kyanula alisema kuwa
pamoja na kuwa kiongozi anayetokana na chama cha upinzani lakini
serikali ni moja hivyo anaungana na wateule wote wa Rais Magufuli katika
kutekeleza dhamira ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo huku
akimtaja Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kama
kiongozi wa mfano katika Mkoa wa Mbeya hivyo kuahidi kushirikiana nae
kwa karibu.
Naibu Meya huyo amempongeza Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kwa kuchangia jumla ya
mifuko 40 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika
shule ya Sekondari Iyera (Mifuko 20) na Shule ya Sekondari Sinde (Mifuko
20) zilizopo Jijini Mbeya.
Alimtaja Mhe Mwanjelwa kwamba amekuwa
mwalimu mzuri wa somo la Uraia Mkoani Mbeya akifundisha kuhusu umoja na
mshikamano huku akisisitiza kuwa Maendeleo ni dhana pana kwa wananchi na
hayapaswi kufanywa kwa mipaka ya vyama vya siasa.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa yupo ziarani Mkoani Mbeya ambapo
amesifu Uongozi wa Wilaya ya Mbeya kwa kazi kubwa katika utendaji
ikiwemo kuanza mchakato wa ujenzi wa vyumba vya madarsa ili kuikabili
changamoto ya wingi wa wananfunzi waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza
Mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment