Mbunge wa Lupa-Chunya Mhe. Masache Kasaka amefanya kikao na wazee wa Chunya kuwaelezea aliyoyafanya toka achaguliwe 2020-2024 kwenye Miradi mbalimbali ya maendeleo.
Pamoja na kikao hicho Mh Masache kasaka aliwapeleka wazee hao kwenda kutembelea na kujionea baadhi ya miradi ambayo imetekelezwa ikiwemo Chuo cha Veta, Uwanja wa Mpira na upanuzi wa jengo la Hospitali ya wilaya ya chunya.
Pia Mbunge Kasaka amemshukuru Mhe Rais Dkt Samia kwa kuendelea kutoa Fedha nyingi za miradi ya Maendeleo kwa Wilaya ya Chunya.
Friday, July 12, 2024
MBUNGE WA LUPA MHE. MASACHE KASAKA AFANYA KIKAO NA WAZEE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment