Social Icons

Tuesday, August 16, 2016

MSAKO WA POLISI WANASA WATUHUMIWA 10 JIJINI MBEYA


Jeshi polisi mkoani Mbeya limefanya msako na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 10 wa uhalifu mbalimbali.
Sehemu ya jiji la Mbeya
Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Zahiri Kidavashari amesema msako huo ulifanyika mnamo tarehe 07.08.2016 hadi tarehe 13.08.2016 katika maeneo ya Uyole, Isyesye, Ituha, Iyela, Airport, Kalobe, Nzovwe, Simike, Forest Mpya na Mwanjelwa.
Amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kuhusika katika matukio ya kupatikana na mali za wizi na kuvunja nyumba usiku na kuiba ambapo majalada ya uchunguzi tayari yamefunguliwa.
Watuhumiwa hao ni pamoja na
1. STEPHANO NAZMA (24) Mkulima na Mkazi wa Ituha
2. REGINA BENEDICT (16) Mkulima na Mkazi wa Kalobe
3. SHABANI DAFA (21) Dereva na Mkazi wa Airport
4. GODFREY NDUKWA (22) Mfanyabiashara na Mkazi wa Airport
5. JAMES ENOCK (20) Mkulima na Mkazi wa Airport.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni
6. FIDELIS NGOVANO (32) Mkulima na Mkazi wa Wilaya ya Mbarali
7. ISRAEL LIYAUMI (33) Mkulima na Mkazi wa Madibila Wilayani Mbarali 8. ZEBEDAYO KADUMA (35) Mkulima na Mkazi wa Uyole
9. RIZIKI ALFEO (17) Mkulima na Mkazi wa Ubaruku Wilayani Mbarali na 10. JOSHUA DAUDI (26) Mkulima na Mkazi wa Ubaruku Wilayani Mbarali.

Ametaja mali na vitu mbalimbali vya wizi vilipatikana kuwa ni:-
Vyerehani vitatu moja aina ya Butterfly,
Amplifier moja,
Spika tatu kubwa,
Laptop aina ya Samsung,
Laptop aina ya HP G.56,
Laptop aina ya HP 693,
Redio aina ya Panasonic,
Television Flat Screen aina ya Boss inchi 32,
Monitor aina ya HP,
Mashine ya Kudarizi ya Umeme,
Viti vitatu vya Plastic,
Keyboard aina ya ACER na Mouse,
Deki aina ya Samsung,
Subwoofer moja aina ya Piano,
Computer isiyokuwa na jina,

Aidha katika zoezi hilo la Misako lilienda sambamba na ukaguzi wa nyumba za kulala wageni zilizopo katika maeneo ya Uyole, Isyesye, Ituha, Iyela, Airport ya Zamani, Kalobe, Nzovwe, Simike, Forest Mpya na Mwanjelwa.
Hali kadhalika wamiliki na wahudumu katika Nyumba hizo za kulala wageni walipewa elimu ikiwa ni pamoja na kuandika majina ya wageni wote katika kitabu cha wageni pamoja na kuweka namba za wahudumu, wamiliki na viongozi wa Jeshi la Polisi kwenye milango kwa ajili ya dharura zitakazojitokeza kwa hatua zaidi.
Kamanda KIDAVASHARI ametoa wito kwa jamii hasa vijana kuacha tabia ya kutaka kupata mali au utajiri kwa njia ya mkato na badala yake wafanye kazi halali ili wapate kipato halali.

CHANZO EATV

No comments:

Post a Comment