Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Serikali
imesitisha kwa muda zoezi la upigaji chapa kwa ng’ombe ili kutoa fusra
kwa wadau kujadiliana na kuona namna bora ya la utekelezaji wa zoezi
husika na kukabiliana na changamoto zilizojitokeza wakati wa
utekelezaji.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi iliyosainiwa
na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bernard Kaali inasema kuwa zoezi hilo
limekuwa likitekelezwa katika baadhi ya mikoa kupitia Mamlaka za
Serikali za Mitaa.
Taarifa
hiyo inasema kuwa zoezi hilo limetokana na sheria Na 10 ya mwaka 2010
ya utambuzi, uandikishaji na utafitiliaji wa mifugo nchini, ambapo
sheria hiyo inalenga kuhakikisha ufugaji unakuwa na tija kwa kuwezesha
mifugo na biidhaa zake kupenya kwenye masoko ya kimataifa.
Aidha,
taarifa hiyo inasema kuwa sheria hiyo inasaidia katika kutatua
changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na watuamiaji wa ardhi pamoja
na kudhibiti masuala ya wizi na kuenea kwa magonjwa ya mifugo.
Pia
inasema kuwa Sheria hiyo inatekeleza uhitaji wa masoko ya kimataifa ya
kuwezesha kufuatilia bidhaatoka kwa mlaji hadi kwa mzalishaji hivyo
endapo zoezi hilo litatekelezwa na wadau na viongozi wa ngazi zote
litakuwa na manufaa kwa wafugaji na taifa kwa ujumla na kupelekea kuleta
mapinduzi katika sekta ya kilimo.
No comments:
Post a Comment