Na: Frank Shija,
MAELEZO.
MAMLAKA husika ya
nidhamu kwa walimu imeagizwa kumvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kutwa ya Sekondari
ya Mbeya, Mwl. Magreth Haule kufuatia kutotoa taarifa juu ya tukio la
kushambuliwa kwa mwanafunzi Kidato cha tatu Shule hiyo Sebastian Chingulu.
Ikizungumza na
mwandishi maalum kutoka Idara ya Habari –MAELEZO, leo Jijini Dar es Salaam
ambapo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. George Simbachawene amesema
kuwa tukio hilo ni la kweli lilitokea tarehe 28 Septemba, 2016 lakini Mwalimu
Mkuu huyo akutoa taarifa, hadi ziliposambaa kwenye mitandao ya kijamii.
“Ninaagiza mamlaka
husika za kinidhamu kumvua madaraka mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbeya
Kutwa Mwl. Magreth Haule avuliwe madaraka kutokana na kukaa kimya huku kukiwa
na tukio la unyama dhidi ya mwanafunzi”. Alisema Simbachawene.
Alisema kuwa kwa
mujibu wa taarifa za awali zilizopatikana tukio hilo lilitokea huku ikidaiwa
chanzo chake ni mwanafunzi Sebastian Chingulu kugomea adhabu aliyopewa na
mwalimu wake.
Aliongeza kuwa walimu
waliohusika na tukio hilo ni wa mazoezi kutoka Chuo Kikuu cha Elimu Dar es
Salaam na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo walishirikiana
kumshambulia mwanafunzi huyo.
SImbachawene
aliwataja walimu hao wa mazoezi kuwa ni pamoja na Frank Msigwa kutoka DUCE,
ambaye ndiye chanzo kikubwa kufuatia madai ya mwanafunzi huyo kugoma kufanya
adhabu aliyopewa na mwalimu huyo.
Wengine ni John Deo na
Sante Gwamoka kutoka DUCE,mwingine ni Evans Sanga kutoka Chuo Kikuu cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Awali akielezea hatua
ambazo tayari Serikali imekwisha zichukuwa, alisema kuwa ni pamoja na Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya kuendelea na ufuatiliaji wa karibu suala
hilo ambapo mpaka sasa vyombo vya dola vinaendelea kuwahoji baadhi ya walimu
washule hiyo.
Hatua nyingine ni
pamoja na kuendelea kuwasaka wahusika wa tukio hilo kwa kuwa mara baada ya
kufanya shambulio hilo walitoweka kusikojulikana, hata hivyo halisisitiza kuwa
hakuna hatakaye kwepa katika hili.
Katika hatua nyingine
Simbachawene aamewaagiza Wakuu wa Shule za Serikali nchini kuzingatia kanuni za
utoaji wa adhabu kwa wanafunzi badala ya kufanya kazi kwa mazoea.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment