Meneja
wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mbeya Mhandisi Charles Irege
(kushoto) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu
(Kulia)mojawapo ya mashine ya uchongaji vyuma iliyo katika karakana
ambayo inahitaji ukarabati.
Picha na Theresia Mwami TEMESA Mbeya.
Na Theresaia Mwami TEMESA Mbeya
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amemuagiza
Meneja wa TEMESA Mbeya Mhandisi Charles Irege kuhakikisha kuwa Mashine
zote zilizo kwenye karakana ya kuchonga vyuma zinafanyiwa ukarabati
ndani ya miezi miwili ili kuongeza uzalishaji.
Dkt.
Mgwatu ameyasema hayo alipotembelea Karakana ya TEMESA iliyopo Jijini
Mbeya na kukuta mashine nyingi za uchongaji vyuma ni mbovu na hazifanyi
kazi.
“Mnakosa
fursa nyingi za kuongeza mapato kwa kushindwa kutengeneza vipuri mbali
mbali vya wateja wakati huu ambapo Jiji la Mbeya linakuwa kwa kasi
kiuchumi” Alisema Dkt.
Dkt.
Mgwatu ameongeza kuwa atafuatilia kwa ukaribu kuona kwamba mashine hizo
za kuchonga vyuma zinafanyiwa ukarabati na kuanza kufanya kazi ipasavyo.
Katika
hatua nyingine Dkt. Mgwatu amemtaka Mhandisi Irege kusimamia vyema
kitengo cha ukodishaji mitambo kilichopo kituoni hapo, kutunza
kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi yatokanayo na ukodishaji mitambo
na kuzuia mianya ya uvujishaji wa mapato ili kukuza pato la TEMESA
Mbeya.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi TEMESA yupo katika ziara ya nyanda za juu
Kusini kutembelea na kukagua vituo vya TEMESA hicho ili kujionea
changamoto na utendaji kazi.
No comments:
Post a Comment