Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa
Na Mwandishi wetu,Chunya
Mkuu
wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa ameitaka halmashauri ya wilaya ya
Chunya kuhakikisha kwamba tozo zote za vijiji za Maliasili zinatozwa na
zinaonekana kwenye taarifa ya mapato na matumizi.
Aidha
ameitaka halmashauri kuingiza takwimu halisi za mazao yote yanayo toka
katika maeneo ya vijiji husika.Agizo hilo, amelitoa leo baada ya
kutembelea na kukagua shughuli za kilimo cha umwagiliaji zinazoendelea
katika skimu ya Ifumbo, ambayo serikali imewekeza kiasi cha shilingi
milioni 900.
Amesema,
licha ya serikali kuwekeza kiasi hicho cha fedha, bado eneo hilo
linakabiliwa na changamoto ya ukusanyaji wa mapato kwani asilimia kubwa
ya mapato hayo yamekuwa hayakusanywi ipasavyo kutokana na kukithiri kwa
njia za panya.
“Serikali
inapoteza fedha nyingi na hii inatokana na kutokuwepo kwa mfumo bora wa
ufutiliaji wa mazao hivyo mchakato huo utasaidia kuongeza mapato katika
Wilaya na halmashauri yenyewe,”amesema.Hata hivyo, amesema nguvu kubwa
iliyopo sasa ni kudhibiti njia zote za panya hasa katika eneo la Shoga
ambalo ndio eneo linalotumiwa zaidi na wafanyabiashara wasio waaminifu.
CHANZO MICHUZI MEDIA GROUP
No comments:
Post a Comment