MBEYA:
Habari kutoka Jijini Mbeya, zimeeleza sema kuwa Mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Mbeya Mjini, Ndugu Ephrahim Mwaitenda mwenye umri wa miaka
(60) amenusurika kifo baada ya kupigwa risasi mgongoni na mtu au watu
wasiofahamika.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,
Emmanuel Lukula amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29. 01. 2017
majira ya saa 05. 45 usiku katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha
Mahenge, Kata ya Makwele, Tarafa ya Ntebela, wilayani Kyela Mkoa wa
Mbeya.
Amesema tukio hilo limetokea wakati
akiwa amelala Kitandani nyumbani kwake Ntebela, ambapo mbinu iliyotumika
ilikuwa ni kukata wavu wa dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za
kienyeji zinazotumia risasi za goroli.
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa, Mwenyekiti huyo amefikishwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na hali yake inaendelea vizuri.
Kamanda Lukula, amewaambia waandishi wa habari kuwa nia ya shambulizi
hilo ilikuwa ni kutaka kumuua na kwamba juhudi za kuwatafuta na
kuwakamata wahusika zinaendelea Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa
Mbeya ndugu Lobe Zongo akimpokea Mwaitenda katika hospitali ya rufaa
Mbeya wakati alipofikishwa hospitalini hapo CCM wilaya ya Mbeya mjini
ndugu Ephrahim Mwaitenda akifikishwa hospitalini hapo
Chanzo : East Africa TV


No comments:
Post a Comment