Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Gabriel Makalla
makamu Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Hoseah Cheyo, akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari wa mkoa huo.
Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dr. Agness Buchwa, akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kuwakabidhi kadi za bima ya afya ya Taifa baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya hawapo pichani..
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akimkabidhi kadi ya bima ya Afya mwandishi wa habari Aines Thobias katika ukumbi wa Coffee Garden uliopo Jijini Mbeya.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa mbeya wakiendelea kudodosa matukio katika hafra fupi ya kupokea kadi za uwanachama wabima ya Afya
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MICHUZI MEDIA MBEYA.
MAELEZO NA GORDON KALULUNGA WA KALULUNGA BLOG
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Gabriel Makalla, amewapongeza waandishi wa
habari mkoa wa Mbeya kwa uamuzi wao wa kuhamasishana kuchangia na
kupatiwa kadi za bima ya Afya ya Taifa (NHIF).
Pongezi
hizo zimetolewa katika ukumbi wa Coffee Garden mjini Mbeya alipokuwa
akikabidhi kadi za bima ya Afya kwa baadhi ya waandishi wa habari Jijini
Mbeya.
Makalla
amesema waandishi wa habari wanafanya kazi kubwa katika Taifa na
waandishi wa mkoa wa Mbeya wameamua kujitambua zaidi na kutambua kuwa
matatizo hayaji kwa kupenda ikiwemo Kifo, Kuugua na uzee.
“Niwakumbushe
wamiliki wa vyombo vya habari kuwawekea mazingira mazuri waandishi wao
na kwamba kuna msemo unaosema kuwa ukondefu wa mbwa ni aibu kwa mwenye
mbwa hivyo kutapatapa kwa waandishi wa habari ni aibu kwa wamiliki”
alisema Makalla.
Aliomba
waandishi kuendeleza uzalendo wao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha
wananchi kujiunga na bima za afya ikiwemo mfuko wa bima ya afya ya jamii
(CHF).
Kwa
upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa
Mbeya Hoseah Cheyo alimwambia Mkuu wa mkoa kuwa pamoja na mambo mengine,
waandishi wa habari wanampongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwa
anazoendelea kuzifanya kwa ajili ya Taifa.
Katibu Mkuu wa chama hicho alisema kuwa waandishi wa habari wamehamasishana wenyewe katika kupata michango na kulipia kadi hizo.
Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dr. Agness Buchwa,
alisema
kwa sasa Hospitali za mkoa wa Mbeya hususani Hospitali ya Mkoa na
Rufaa, wametenga maeneo maalum kwa ajili ya watu wanaotibiwa kwa njia za
kadi za bima ya Afya.
Mwakilishi
wa Meneja wa mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Haji Mpeta alisema kuwa
matibabu ni ghali hivyo waandishi waliolipia kadi za bima ya Afya
wataweza kupata matibabu katika vituo 6500 kote nchini kwa gharama ya
Tsh. 76,800 kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment