Na Zawadi Msalla-WHUSM
Viongozi
wa kimila Mkoani Mbeya waunga mkono juhudi
za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hatua mbalimbali za kuhakikisha
Tanzania inafika katika uchumi wa kati wa Viwanda .
Wameyasema
hayo walipokuwa wakizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel katika
ziara yake Mkoani humo na kuongeza kuwa ni vema Watanzania waungane kwa pamoja kufanikisha nia njema ya Rais, Dkt. Magufuli.
Akizungumza
kwa niaba ya viongozi hao ,Chifu Rocket Mwashinga kutoka Igawilo alisema kuwa Rais
anasisitiza wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na umaskini na
kulijenga taifa.
“Tufikishie
ujumbe huu kwa Mhe. Rais ili hao vijana wetu wanaokimbilia mijini badala ya
kukaa na sisi wazee kulima nchi isiwe na njaa warudishwe vijijini waje walime
na kwa maendeleo yao binafsi na taifa”
“Inasikitisha sana kuona siku hizi vijana wakilalamikia
Serikali kuwa maisha ni magumu wakati wameacha mashamba na wao ndiyo watu wenye
nguvu ambapo magenge makubwa ya ujambazi, wabakaji na walevi waliopitiliza yaliyopo huko mijini yanatokana na vijana
wasio na ajira” Alisema Chifu Mwashinga.
Aidha
Wakuu hao wa kimila walieleza kuwa ili kauli mbiu ya Hapa Kazi tu iweze kutekelezeka wameiomba Serikali iangalie
utaratibu wa kuwarudisha vijijini vijana wasio na ajira waliopo mijini kwa kuwa
wao ndio nguvu kazi na chachu ya
maendeleo.
Pia
viongozi hao waliishauri Serikali kufufua kilimo shuleni ambapo hapo awali
watoto walifundishwa elimu ya kujitegemea kwa kulima mashamba na kujenga majengo ya shuleni mambo ambayo kwa
sasa hayafanyiki.
“Tulifundishwa
kupenda kilimo tukiwa shuleni ,watoto wa siku hizi hata jembe hawajui
kulishika” Alieleza Chifu Joseph Mwalawa.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel aliiomba ofisi ya
Mkuu wa Mkoa kuwatambua wakuu hao wa kimila ili kwa pamoja waweze kusukuma
gurudumu la Maendeleo ya taifa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment