Akizungumza jana, Mratibu wa ziara hiyo, Kassa Mussa alisema kuwa Bella atafanya onyesho lake la kwanza kesho kwenye Ukumbi wa City Pub ulioko jijini Mbeya na ataimba vibao vyake vipya na vya zamani vilivyowahi kutamba.
Mussa alisema baada ya onyesho hilo, Bella ambaye ameambatana na bendi yake ya Malaika, keshokutwa watatumbuiza kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, uliopo Sumbawanga mjini Rukwa na atamaliza ziara ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Jumapili mjini Tunduma.
"Maandalizi yamekamilika na kila kitu kinakwenda vyema, Bella amejiandaa kuonyesha burudani ya kimataifa kwa sababu anajua fursa hii itamsaidia kuongeza mashabiki ambao hawajamuona kwa muda mrefu," alisema mratibu huyo.
Aliongeza kuwa kila onyesho ambalo Bella hufanya mikoani huwaandalia mashabiki wake vitu vipya kwa lengo la kuonyesha ukongwe kwenye kazi hiyo ambayo aliianza zaidi ya miaka 10 iliyopita.

No comments:
Post a Comment