Kaimu
Jaji Mkuu Wa Tanznaia Mhe. Prof. Ibrahim Juma Akifungua Pazia Kuashiria
Uzinduzi Wa Mahakama Ya Watoto Leoi Jijini Mbeya. Katikati Ni
Mwakilishi Wa Unicef Nchini, Stephanie Shanler Na Kushoto Ni Jaji
Kiongozi Wa Mahakama Kuu Ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali.
Kaimu Hjaji Mkuiu Wa Tanznaia Mhe. Porof. Ibrahim Juma Akikata Utepe Kuzindua Jengo La Mahakama Ya Watoto Leo Jijini Mbeya.
Kaimu Jaji Mkuu Wa Tanznaia Akizungumza Wakati Wa Hafla Hiyo
Kaimu
Jaji Mkuu Wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma Akiwa Katika Picha Ya
Pamoja Na Viongozi Wa Mahakama Ya Tanzania Mara Baada Ya Kuzindua
Mahakama Ya Watoto Leo Jijini Mbeya
Msajili
Mkuu Wa Mahakama Ya Tanzania Mhe. Katarina Revokati Akiwa Pamoja Na
Mwakilishi Wa Unicef Nchini, Stephanie Shanler Na Jaji Wa Mahakama Kuu
Mbeya Mhe. Mary Levira Wakati Wa Uzinduzi Wa Mahakama Ya Watoto.
Jaji Mfawidhi Wa Mahakama Kuu Kanda Ya Mbeya Mhe. Noel Chocha Akizungumza Wakati Wa Hafla Hiyo
Na Lydia Churi
Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma leo amezindua rasmi
Mahakama ya watoto katika jiji la Mbeya na kufanya idadi ya Mahakama
hizo nchini kufikia mbili. Mahakama ya kwanza ya watoto iko Kisutu
jijini Dar es salaam.
Mahakama
hii ya Watoto iliyoanza kufanya kazi rasmi Aprili 18 mwaka huu jijini
Mbeya pamoja na ile ya Kisutu zina kazi kubwa ya kuamua kesi za watoto
wanaojikuta wana ukinzani na Sheria zinazohusu watoto nchini pamoja na
kutafsiri sheria hizo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania alisema maendeleo
endelevu ya Tanzania yatajengwa kwa misingi ya haki za watoto huku
akinukuu andiko la shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na
watoto (UNICEF) lisemalo maendeleo ya taifa lolote yatakamilika baada ya
watoto kuwa na afya njema, salama pamoja na kupata elimu.
Alisema
uzinduzi wa jengo la Mahakama hiyo ya watoto unaashiria safari ndefu
iliyonayo Tanzania ya kuhakikisha haki za watoto zinalindwa kwa kuwa pia
bado kuna mikoa mingi ambayo inahitaji huduma hii muhimu.
Prof.
Juma alisema kazi kubwa ya Mahakama ya Tanzania ni kutoa tafsiri pana
ya sheria zinazohusu haki za watoto ili kupanua wigo wa ulinzi kwa
watoto huku akiwataka Majaji na Mahakimu nchini kutafsiri sheria hizo
ili zitekeleze wajibu wao kisheria.
Akitolea
mfano wa Sheria ya Watoto namba 21 ya mwaka 2009, Kaimu Jaji Mkuu
alisema sheria hii inashirikisha mihimili yote mitatu hivyo haki zote
zinazotajwa na sheria hii ni lazima zipatikane inavyostahili. Prof. Juma
pia amewataka Mahakimu wanaosikiliza kesi za watoto kuainisha mapungufu
ya sheria hii na kuyawasilisha kwenye kamati ya Jaji Mkuu inayohusu
masuala ya Sheria.
Aidha,
Kaimu Jaji Mkuu amewataka Majaji na Mahakimu nchini wanaosikiliza kesi
za watoto kujisomea zaidi masuala yanayohusu maendeleo ya haki za watoto
kwa kuzisoma taarifa za utekelezaji za nchini pamoja na zile za nchi
nyingine ili kupanua uelewa wa sheria hizo.
Kaimu
Jaji Mkuu pia amewataka Majaji na Mahakimu wote kusimamia na
kuhakikisha masuala yote yaliyotajwa na Sheria pamoja na mikataba ya
kimataifa kuhusu watoto yanatekelezwa pindi wanapofanya ukaguzi kwenye
magereza mbalimbali.
Wakati
huo huo, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand
Wambali amewaomba UNICEF kufikiria na kuangalia uwezekano wa kujenga
majengo mengine manne ya mahakama za watoto katika mikoa ya Arusha,
Mwanza, Dodoma na Tabora ili kuwapatia Mahakimu fursa ya kujifunza kwa
vitendo namna Mahakama za watoto zinavyofanya kazi.
Jengo
la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya lililojengwa kwa ushirikiano kati ya
Mahakama ya Tanzania na UNICEF limegharimu kiasi cha shilingi za
kitanzania milioni 415 ambapo Mahakama imechangia kiasi cha shilingi
milioni 214 na UNICEF shilingi milioni 201.
No comments:
Post a Comment