Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe
amewashukuru viongozi wote wa Serikali, Sekta binafsi, Taasisi za Kidini
vyombo vya habari na watanzania wote waliomfariji katika msiba wa mke
wake Bibi Linah Mwakyembe uliotokea Julai 15 mwaka huu.
Akizungumza
wakati wa Misa ya mazishi ya mke wake huyo iliyofanyika jana nyumbani
kwake Kyela Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa amefarijika sana kwa upendo
ulioonyeshwa na kila mtu kwa nafasi yake katika kipindi hiki kigumu na
kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kila jambo.
“Mimi na
wanangu tumefarijika sana kwa kuona jinsi ambavyo Watanzania na wana
Kyela mlivvyokuwa na upendo kwetu mmetupa faraja na mmetutia nguvu na
mmetuoshesha ushirikiano mkubwa katika jambo hili tunaomba mwenyezi
Mungu awabariki sana na asanteni sana”Alisema Mhe Waziri Mwakyembe.
Kwa
Upande wake Mhe.Amos Makala Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakati akitoa salamu
za pole kwa niaba ya wanachi wa mkoa wake amesema wananchi wa Mbeya
watamkumbuka marehemu mama Linah Mwakyembe kwa moyo wake wa kujitolea
kusaidia jamii katika mambo mbalimbali ikiwemo kufundisha jamii kumcha
Mungu pamoja na Ujasiriliamali uliosaidia wanawake wa Kyela kujiajiri.
“Wananchi
wa Mbeya tunakupa pole sana Mhe. Mwakyembe pamoja na familia yako
lakini pia tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya mama Linah hapa
duniani ambayo yameleta faida kwa jamii tunamuomba mwenyezi Mungu amlaze
mahala pema peponi amina lakini na wewe pia tunakuombea Mungu aendelee
kukupa uvumilivu na uamini kuwa hili nalo litapita”.Alisema Mhe Makala.
Marehemu Bibi Linah Mwakyembe ameagwa na kuzikwa jana nyumbani kwake Kyela na ameacha watoto watatu.
No comments:
Post a Comment