Mdadisi
kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akihoji taarifa za kaya wakati
wa zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi
ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaloendelea kufanyika
nchini ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi
karibuni.
Mdadisi
kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akihoji taarifa za kaya wakati
wa zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi
ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaloendelea kufanyika
nchini ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi
karibuni.
Mdadisi
kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akiwaoneyesha wasimamizi namna
alivyojaza taarifa za kaya wakati wa zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili
ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka
2017/18 linaloendelea kufanyika nchini ikiwa ni maandalizi ya utafiti
huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA)
Na: Veronica Kazimoto
ZOEZI
la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya
Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaendelea nchi nzima ikiwa ni
maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni.
Akizungumzia
zoezi hilo, Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu, Sylvia Meku wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu amesema mpaka sasa mikoa kumi na tatu (13)
imekamilisha zoezi hilo ambapo ni sawa na silimia 50.
“Zoezi
la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya
Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaendelea vizuri na mpaka sasa
wadadisi wamekamilisha kuorodhesha kaya katika mikoa 13,” amesema Sylvia
Meku.
Ameitaja
mikoa iliyokamilisha zoezi la uorodheshaji wa kaya kuwa ni pamoja na
Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Iringa, Njombe na Morogoro. Mikoa
mingine ni Mwanza, Tabora, Katavi, Mbeya, Mara, Kagera na Lindi.
Zoezi la Uorodheshaji wa Kaya linafanyika mikoa yote ya Tanzania Bara na linatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi Julai, 2017.
Utafiti
kama huu mara ya mwisho ulifanyika Mwaka 2011/12 ambao ulionesha kuwa
asilimia 28.2 ya Watanzania wanaishi chini ya mstari wa Umaskini wa
mahitaji ya Msingi.
Utafiti
wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18
unafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya
Fedha na Mipango na baadhi ya Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kupata
viashiria vya kupima hali ya umaskini nchini.
No comments:
Post a Comment