Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa
(Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa kilimo akimnadi Mgombea Udiwani Kata ya
Ibigi Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya Bi Suma Ikenda Fyandomo, Jana
Novemba 20, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa
(Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa kilimo akimvalisha kofia ya CCM kijana
aliyehama Chadema wakati wa kampeni za Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani
Rungwe Mkoa wa Mbeya Bi Suma Ikenda Fyandomo, Jana Novemba 20, 2017.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa
(Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa kilimo akifurahi na wananchama wa CCM
wakati wa mkutano wa kumnadi Mgombea Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani

Na Mathias Canal, Mbeya
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa
(Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo amewasihi wananchi kwa kauli
moja kuchagua kiongozi makini anayetokana na CCM.
Mhe
Mwanjelwa alisema kuwa kumchagua diwani wa CCM ni dalili nzuri ya
kumpongeza na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anazozifanya kwa muktadha
wa kuwaletea maendeleo watanzania wote.
Mjumbe
huyo wa NEC, aliyasema hayo Leo Novemba 20, 2017 katika Mkutano wa
hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Bujinga A na B kilichopo Kata ya
Ibigi, Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya ambapo alimnadi mgombea Udiwani wa
Kata hiyo Bi Suma Ikenda Fyandomo.
(Mnec),
Mhe Mwanjelwa aliwakumbusha wananchi waliojitokeza katika mkutano huo
kuwa Hawachagui ilani mpya Bali wanachagua Diwani kwa ajili ya
kutekeleza ilani ya Ushindi ya CCM ya Mwaka 2015-2020 ambayo wananchi
waliiamini na kuichagua Octoba 25, 2015.
Alisema
kuwa nchini Tanzania hakuna chama chenye uwezo wa kuwaletea maendeleo
wananchi Bali Chama Cha Mapinduzi pekee ndicho chenye uwezo na jukumu la
kuwaletea maendeleo endelevu wananchi.
Katika
Mkutano huo wanachama 21 walivutiwa na hotuba ya Mjumbe huyo wa
Halmashauri kuu ya CCM wakati akimnadi mgombea hivyo kufanya maamuzi ya
kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM ambapo wameahidi
kushirikiana na mgombea udiwani wa CCM ili kuhakikisha anashinda kwa
kishindo.
Ushiriki
wa kampeni hizo katika Kata ya Ibigi unajili wakati ambapo Naibu Waziri
wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa yupo ziarani Mkoani Mbeya ambapo pamoja na
mambo mengine Kesho Disemba 21, 2017 atashiriki ufunguzi wa Mkutano wa
Makatibu Tawala na washauri wa kilimo wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
juu ya mfumo wa ununuzi wa mbolea (BPS).
Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa Jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment