Social Icons

Tuesday, November 21, 2017

USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA MBEYA


Wananchi wa Kata ya Mwakidete mtaa wa Mwakibete mkoani Mbeya wakiendelea na Usajili Vitambulisho vya Taifa.
Mmoja wa wananchi wa Mtaa wa Mwakibete akiweka saini kwenye mashine maalumu ya uchukuliaji alama za kibaiolojia, picha na saini ya kielektroniki.
Wanaoonekana kwenye picha ni Baadhi ya Maafisa Usajili wa NIDA wakiendelea na zoezi la kuwasajili wananchi wa Kata ya Mwakidete mkoani Mbeya. Kushoto ni Afisa Usajili Wilaya ya Mbeya Bi. Alavuya Ntalimwa akitabasamu jambo na wananchi wa Mtaa wa Mwakibete.
Mwananchi akichukuliwa alama za Vidole na afisa Usajili wa NIDA wakati zoezi la kuwasajili wanannchi likiendelea. 
Msururu wa wananchi wa Mtaa wa Mwakibete wakisubiri huduma ya usajili.

Mamlaka ya Vitambuisho vya Taifa (NIDA) inaendelea na zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu mkoani Mbeya ambapo wananchi wengi wamejitokeza ambapo kwa sasa usajili unaoendelea niwa mkupuo (mass registration) ambapo wananchi wanakusanyika kwenye mitaa na vijiji wanakoishi kusajiliwa ambapo Usajili huo unahusisha ujazaji fomu, uchukuaji alama za vidole picha na saini ya kielektroniki. 

Akitoa elimu kwa umma kuhusu taratibu za Usajili mwakilishi wa kitengo cha Mawasiliano NIDA Bw. Deodatus Alexander Mchaki amesema zoezi hilo ni fursa ya kipekee kwa wananchi kutambuliwa na kusajiliwa.

Amesisitiza zoezi la usajili ni Bure na wananchi hawatakiwa kutozwa gharama zozote Ili kusajiliwa mwananchi ni lazima afike na nakala (photocopy) ya nyaraka/viambatisho vifuatavyo kuthibitisha Umri, Uraia na Makazi yake ikiwemo cheti cha kuzaliwa, Passport (Pasi ya kusafiria), Kadi ya kupigia kura, leseni ya udereva, ID ya Mzanzibar mkazi, TIN, Pasi ya kusafiria na vyeti vya elimu.

No comments:

Post a Comment