Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua mawe yaliyo katwa, Kusagwa na kuongezewa thamani katika kiwanda cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal, Wazo Huru Blog
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasili katika kiwanda kinachoshughulika na kukata, Kusaga na kuuza mawe cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Ndg Salim Jesa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Marmo E. Granite Mines (T) Ltd kuhusu usafirishaji wa mawe baada ya kuyaongezea thamani wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua utendaji kazi wa kiwanda cha kukata, Kusaga na kuuza mawe cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Mbeya
Wamiliki wa leseni za madini ya dhababu, vito na mengineyo kote nchini wametakiwa kuiga mfano wa Ndg Salim Jesa mmiliki wakiwanda
cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd kinachojishughulisha na kukata,
Kusaga na kuuza mawe kwa kufanya mchakato mzima mpaka bidhaa kukamilika
hapa hapa nchini.
Kauli
hiyo kwa wamiliki wa leseni za madini nchini imetolewa leo 20 Februari
2018 na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati
akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati akiwa katika ziara ya
kikazi Mkoani Mbeya.
Alisema
kuwa kiu ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ni kuona rasilimali
za nchi zinaongezwa thamani zikiwa ndani ya nchi jambo ambalo linaakisi
umakini wa utendaji na ulipaji kodi ya serikali pasina kukwepa ama
kutorosha rasilimali madini yakiwa ghafi.
Aliseama
kuwa faida ya kuongeza thamani ya madini nchini ndio muarobaini wa
sekta ya madini kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la Taifa
hatimaye kufikia asilimia 10% kama ulivyo mpango wa wizara kuongeza
kiwango cha uchangiaji wa pato la Taifa.
“Nchi
nyingi ambazo zimejua siri hii kwa kiasi kikubwa zimefanikiwa lakini
sisi Tanzania tulichelewa sana, na kama tungeendelea kuchelewa ingefika
kipindi ambacho madini yasingekuwepo kamwe na kama Taifa tungeambulia
mashimo makubwa na kusalia katika wimbi la umasikini” Alisema Mhe Biteko
Aidha,
amemuhikishia mmiliki wa kiwanda hicho kuwa serikali itazungumza na
taasisi zinazofanya kazi za ujenzi nchini kuunga mkono juhudi za umahiri
wa kiwanda hicho kwa kununua bidhaa zinazozalishwa hususani wakati huu
ambao serikali inaendelea na mchakato wake wa kuhamia Mjini Dodoma.
Sambamba
na hayo pia uongozi wa kiwanda hicho umempongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweka sera nzuri
hususani kwa wawekezaji wa ndani katika sekta ya madini na juhudi zake
za kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na serikali kwa ujumla wake.
Kampuni
ya Marmo E. Granite Mines (T) Ltd iliyopo mkoani Mbeya ilianzishwa
mradi wa kukata, kusaga na kuuza mawe Januari 2004 baada ya kukidhi
masharti ya usajili wa makampuni.
No comments:
Post a Comment